Update:

Raia 35 wa Ethiopia washtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya kigaidi
Raia 35 wa Ethiopia wamefikishwa mahakamani nchini humo kwa kosa la kuchochea vurugu na kujaribu kufanya vitendo vya kigaidi kati ya mwaka jana na Januari mwaka huu kwa niaba ya kundi la kigaidi la Patriotic Front.

Washukiwa hao wanatuhumiwa kufanya vitendo hivyo kwa kubeba silaha katika maeneo ya kaskazini na kusini mwa Gondar mkoani Amhara.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanatuhumiwa kushambulia raia, mashirika ya umma na maofisa usalama kwa kuandikisha wafuasi wengine na kupokea ufadhili wa dola za kimarekani elfu 34,528 kutoka kwa viongozi wa kundi hilo walioko nchi za Marekani, Ujerumani, Sweden, na hasimu wake mkuu Eritrea.