Update:

PAMPU YA PLASTIKI INAYO VUTA MAJI KUTOKA ARDHINI YAGUNDULIKA ARUSHA
Omala akijaribu kuonyesha namna ya kupampu maji baada ya kukamilisha ujenzi wa pampu hiyo Katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira wa kukata miti na kuchoma matofali maeneo mbalimbali nchini baadhi ya wananchi wamebuni njia nyingine mpya ya kuweza kuepukana na uharibifu huo kwa kugundua matofali yenye uwezo wa kuchomana yenyewe hali ambayo inapunguza matumizi ya kuni pamoja na kuharibu mazingira.
Muandisi Petro Omala  Kulia akimuonjesha Mwandishi wa habari hii Aina ya tofali lenye uwezo wa  kuchoma matofali mengine


Petro Omala mkazi wa Elerai jijini Arusha ni mbunifu wa vitu mbalimbali ambapo ameweza kubuni kisima cha maji chenye uwezo wa kuhudumia jamii kubwa katika kata hiyo huku pia akiwa anamiliki kiwanda kidogo cha kuchoma matofali ambacho hakitumii kuni huku akieleza kuwa aliweza kupata matofali yenye uwezo wa kuhifadhi joto pindi yakichomwa na kuweza kutumika kuchonma matofali mengine

Pamoja na kuzungumzia jinsi alivyoweza kubuni mambo hayo petro Omala akazungumzia kisima cha maji ambacho kimechimbwa kwa mikono huku bomba lake likwa ni mpira ambapo pia yanatumika kwa wananchio wanaoishi jirani na eneo hilo.

Mara baada ya kuweza kuzungumza na mbunifu huyo ambaye ana zaidi ya miaka 70 kwa upande wao wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo na kuweza kunufaika na maji hayo wakaeleza jinsi hali ya upatikanaji wa maji ilivyokuwa awali tofauti na kipindi sasa ambapo wamepata huduma hiyo.


Wakati wananchi wakiwa wanabuni njia za kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kukta miti na kuchoma matofali inakuja huku kukiwa na wimbi kubwa la uharibifu wa mazingira kwa wananchi kukata miti na kuchoma matofali hali ambayo inadaiwa kuchangia uharibifu wa mazingira.

No comments