Update:

Ni rasmi sasa Haruna Niyonzima hataendelea na klabu ya Yanga

Baada ya habari nyingi za muda mrefu kuhusiana na hatma ya kiungo wa kimataifa wa Rwanda anayeichezea Dar es Salaam Young Africans Haruna Niyonzima kuhusishwa kuhama Yanga na kujiunga na Simba baada ya mkataba wake kumalizika, jana Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa alitangaza na kuweka wazi kuwa mchezaji huyo ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika July, wameshindwa kufikia makubaliano ya kumuongezea mkataba mpya.

Hivyo ni rasmi sasa baada ya Haruna Niyonzima kuitumikia Yanga kwa misimu sita mfululizo, atakuwa nje ya Yanga kuanzia msimu ujao wa 2017/18, bado haijajulikana rasmi Niyonzima atajiunga na timu gani lakini kwa tetesi zinazoenea ni kuwa Niyonzima atajiunga na Simba.

No comments