Update:

Nashangaa watu wanaosema nimemkimbia P-Funk – Jay MoRapper Mabeste amesema kwa sasa yupo tayuari kujiunga na lebo yoyote ya kusimamia muziki.Mabeste ambaye alikuwa chini ya B Hits Music Group kipindi cha nyuma, amesema muziki wake unahitaji usiamamizi. Msanii huyo amekiambia kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM hawezi kutaja ni label ipi anahitaji bali ni watu walio makini ndio atakuwa tayari kufanya nao kazi.

“Natamani kudeal na record label yoyote au kampuni yoyote ambayo inadeal na artist the way tutakavyokubaliana. Siwezi kusema kwamba nita deal na watu fulani au watu fulani ndio wapo sawa, hapana ni the way tutakavyokubalian,” amesema Mabeste.

“Kikubwa zaidi nini wanafanya na nini nitafanya ndicho ninakiangalia sana na the way wao watakavyo nionyesha ndicho kitafanya mimi niweze kuvutika kufanya kazi nao. Mimi siangalii mtu, naangalia utendaji wa kazi ukoje,” ameongeza.

No comments