Update:

Nashangaa watu wanaosema nimemkimbia P-Funk – Jay MoHitmaker wa Nisaidie Kushare, Jay Mo amesema anawashangaa watu wanaodai kumkimbia mtayarishaji wa muziki mkongwe nchini, P-Funk kutoka studio za Bongo Records.Jay amesema kufanya kazi mbili na maproducer tofauti na Majani siyo ndio kamkimbia kwani hata kwenye hizo kazi mtayarishaji huyo kuna mchango wke mkubwa.

“Nashangaa watu wanasema nimekimbia kwa P-Funk, kisa ngoma mbili nimefanya na maproducer tofauti. Yaani hawajui kuwa hata ile ngoma niliyofanya na Daz Knowlege nimefanya Bongo Record, producer alikuja pale tukarekodi pale,” amesema Jay Mo katika kipindi cha Playlist cha Times FM.

“Unadhani P asingeniami angeruhusu producer mwingine kutumia studio yake?,” ameongeza.

No comments