Update:

Mkurugenzi Mkuu Ewura asimamishwa kazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura ), Felix Ngamlagosi. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema Ngamlagosi amesimamishwa kazi kuanzia leo (Jumapili) Juni 11. Ngamlagosi aliteuliwa kushika wadhifa huo Februari Mosi, 2014 akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Haruna Masebu, aliyemaliza muda wake Desemba 31, 2013 akiwa ameitumikia mamlaka hiyo kwa vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja kwa mujibu wa Sheria ya Ewura. Kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, Ngamlagosi alikuwa Mkurugenzi wa Udhibiti wa Kiuchumi wa Ewura, nafasi aliyokuwa ameitumikia kwa miaka saba.

No comments