Update:

Manchester City yamsajili kipa Ederson Moraes


Timu ya Manchester City imefikia makubaliano ya kumsajili kipa Ederson Moraes, toka klabu ya Benfica ya Ureno na kuwa usajili wa pili wa Man City baada ya ligi kumalizika.

Uhamisho wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 umeigharimu City kitita cha paundi milioni 35 na kumfanya kuwa kipa wa pili ghali katika historia baada ya Gianliugi Buffon aliposajiliwa na Juventus

akitokea Parma mwaka 2001.

Ederson alikwenda Manchester katika uwanja wa mazoezi wa City kukamilisha vipimo vya afya na kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya klabu.

City sasa wanakuwa wameshatumia kitita cha paundi milioni 78, baada ya klabu hiyo kumsajili na kumnasa kiungo Bernardo Silva kwa kitita cha paundi milioni 43 kutoka Monaco.

No comments