Update:

Mamlaka ya hifadhi nchini Tanzania yaanza utalii rafiki ili kuvutia zaidi watalii


Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro nchini Tanzania imeanza aina mpya ya utalii inayolenga kuboresha utalii unaojali mazingira ili kuvutia zaidi watalii.
Mhifadhi Mkuu wa mamlaka hiyo Freddy Manongi amesema, aina hiyo mpya ya utalii inalenga kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea eneo hilo la utalii linalotambuliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), lililoko kilomita 180 kutoka mji wa Arusha nchini Tanzania. Amesema mamlaka hiyo imeshatambua maeneo ya utalii unaozingatia mazingira ikiwemo milima, maeneo ya kijiografia, na maeneo ya kale, ambayo yalianzishwa miaka 58 iliyopita.

No comments