Update:

Jinsi ya kutafuta kazi kwa ufanisi mtandaoni

Kutafuta kazi inaweza kuchukuwa mdaa mrefu, na ikakufanya uwe na msongamano wa mawazo. Miakaa kadhaa iliyopita kulikuwa kuna namna chache sana za kutafuta kazi, ilikuwa  uangalie magazetini au uwende maofisini kuacha CV zako. Siku hizi na uboresho wa teknolojia, imerahisisha jinsi watu wanavyo tafuta kazi.
keyboard-417090_960_720

Tengeneza akaunti
Ili uweze kuanza kutafuta kazi na kutuma maombi katika mtandao wetu, inabidi utengeneze akaunti yako bure ambayo mwajiri ndiyo ataiona kila ukituma maombi ya kazi. Ukifika kwenye tovuti yetu ya Jumia Jobs ni rahisi kujisaliji, bofya kwenye sehemu iliyoandika “Sign Up” na uanze kutengeneza akaunti yako. Jaza maelezo yako yote, hakikisha umejieleza vizuri. Maelezo yako yakiwa yamekamilika ni rahisi zaidi kumvutia mwajiri.
Angalia Barua pepe
Baada ya kutuma maombi yako kwenye nafasi tofauti tofauti kwenye mtandao, unaweza pata barua pepe itayokuambia kama muajiri anangalia CV yako. Inabidi uhakikishe kwamba unangia kuangalia barua zako pepe mara kwa mara. Kuna waajiri wengine hawapigi simu ila wanatuma barua pepe na kukuambia labda ujibu maswali au ufanye mtihani kabla ya kwenda kwenye mahojiano. Ni vizuri pia kuangalia barua pepe kwasabu kila wiki Jumia Jobs tunakutumia barua pepe mara 3 kwa wiki kuhusu nafasi mpya zilizokuwepo kwenye tovuti yetu.
Tembelea tovuti za kazi mtandaoni
Kupata kazi hapo kwa hapo ni kitu kigumu sana, ila usikate tamaa. Uwe una tembelea tovuti yetu mara kwa mara na utume maombi ya kazi sehemu mbali mbali. Kila siku tenga kama lisaa limoja na uwe unatembelea tovuti mbali mbali za kazi.

Kumbuka hamna kitu kina kuja kirahisi rahisi na kitu kiki shindikana mara ya kwanza usikate tamaa. Kutafuta kazi ni kitu kinacho chukuwa mdaa, inabidi uwe una subira.
Asante!