Update:

Jinsi ya kupata ajira katika kampuni, baada ya kuifanyia kazi kwa kujitolea


Kutafuta kazi baada ya kuhitimu chuo inakuwaga ngumu. Unaweza ukawa hujawai kusikia au kuona matangazo yano husika na kazi za kujitolea (internship). Tuna habari nzuri kwajili yako, kazi za kujitolea zinaweza kuwa njia nzuri sana kwajili ya kupata ajira ya kudumu.Maana ya internship: ni kazi ya mudaa ambayo unajitolea katika kampuni, inaweza ulipwe au usilipwe. Mara nyingi huwa hizi nafasi zinatolewa kwa watu walio hitimu chuo na wanatafuta kupata ujuzi katika sekta waliyosomea. Nakala hii itakupa ufafanuzi ya jinsi ya kupata ajira baada ya internship.

Wakati uko katika internship, fanya bidii kujua kila kitu kuhusu kampuni. Jua kila kitu kuhusu kitengo chako, Jaribu kuulizia jinsi ya kuweza kupata ajira baada ya kumaliza internship yako. Onyesha kwamba unapenda kazi yako na unaweza ukaisaidia kampuni kukuaa.

Wakati uko kwenye internship, inabidi uzoeane na wafanya kazi wenzio, ujenge ukaribu na urafiki nao. Jua kazi wanazofanya, jifunze kwao. Ikifika mwisho wa internship yako, mwajiri anaweza akawauliza wafanya kazi wenzako kama unafaa kubaki kwenye kampuni.

Hakikisha unatumia mdaa wako vizuri, fanya kazi kwa bidii na uwe muaminifu, uonekane kwamba unaweza ukafaa kufanyia kazi kampuni moja kwa moja. Uwe msikivu, fwata vigezo utakavyopewa na bosi au wafanya kazi wenzako. Kuwa mbunifu kwa kila utachokifanya, hakikisha kila kazi unayopewa unaifanya kwa wakati. Usilalamike ukipewa kazi nyingi, au kama ukiwa huna kazi usisite kuomba kupewa kitu cha kufanya.

Ukipata wazo zuri, linaloweza saidia kampuni usiogope kuongea. Ita muonyesha mwajiri kwamba unataka kampuni iwe na maendeleo mazuri. Ukiulizwa kuhusu mipango yako ya kazi, usisite kusema kwamba ungependa kuendelea kufanya kazi katika kampuni hiyo hiyo na jinsi gani inaweza fanyika.