Update:

Di Maria akumbwa na mkasa wa kukwepa kulipa kodi

Wakati kashfa ya ukwepaji kodi ikiwaandama Wareno wawili maarufu, Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho, kumeibuka nyingine ambapo Angel Di Maria naye amekumbwa na mkasa kama huo.

Di Maria amekiri kuhusika na ukwepaji kodi kati ya mwaka 2010 na 2014 akikwepa kulipa kodi kiasi cha euro milioni 1.14.

Inasemekana baada ya kugundua kwamba amefanya kosa hilo, Di Maria aliamua kupanga njama na baadhi ya watu wa mamlaka za kodi ili kosa lake lisijadiliwe. Baadae polisi waliamua kuingilia kati suala hilo na kuanza kumchunguza upya ambapo mwisho alikiri mbele ya sheria kwamba alifanya kosa hilo.

Di Maria alikiri pia kutumia akaunti mbili alizozitumia kukwepea kodi na kila akaunti inamfanya kuhukumiwa miezi 6 jela na hivyo kuhukumiwa miezi 12 jumla na kulipa faini ya 60%.

Lakini Di Maria hatakwenda gerezani, kwani sheria za Hispania hazimpeleki gerezani mtu aliyehukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili haswa kama hajawahi kufungwa hapo kabla na Di Maria atatumikia kifungo cha nje.

No comments