Update:

Chile yapaa hadi fainali kombe la mabara

Mchezo kati ya mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Chile ambao ni mabingwa wa Amerika uliokuwa wa shika nikushike kama ilivyotarajiwa na wengi umeipeleka Chile katika hatua ya fainali.

Mchezo huo wa nusu fainali ya confedaration cup ulimalizika dakika 90 kukiwa hakuna timu iliyopata bao na hata zilipoongezwa dakika 30 ili kumalizia 120 milango bado ilikuwa ni migumu.

Baada ya hapo muamuzi aliamuru kupigwe mikwaju ya penati ambapo Ureno waliondolewa baada ya Chile kufunga mikwaju yote mitatu ya mwanzo ya penati huku Wareno wakikosa.

Shukrani kwa mlinda mlango wa Chile Claudio Bravo ambaye aliokoa penati tatu za Ricardo Quaresma, Moutinho na Nanj huku za Chile zikiwekwa kamiani na Vidal, Sanchez na Aranguiz.

Baada ya mchezo huo ambao Bravo anayeidakia Man City kuwa mchezaji bora wa mechi sasa Chile wanakwenda fainali wakisubiri mshindi kati ya Ujerumani na Mexico kwa ajili ya fainali hiyo ya Confedaration Cup.

No comments