Update:

Chidi Benz kurudi upya na wimbo ‘Muda’ akiwa na Q Chief


Baada ya kujikomboa kutoka katika matumizi ya dawa za kulevya rapa Chidi Benz amejipanga upya ambapo wiki ijayo ataachia wimbo wake uitwao Muda akiwa amemshirikisha muimbaji Q Chief.Uongozi mpya wa rapa huyo umesema kuwa kazi hiyo mpya ya rapa huyo imeandaliwa ndani ya studio za Kill Record chini ya producer Mbezi.

“Wiki ijayo Chidi Benz anarudi upya kwenye game, ngoma ni kali sana bila shaka mashabiki walikuwa wanamsubiria Chidi yule wazamani,” alisema meneja huyo aitwae Shabaha. Mimi binafsi nje ya umeneja Chidi ni msanii ambaye namkubali sana toka kitambo, nilivyosikiliza hii kazi yake mpya akiwa amemshirikisha Chidi Benz nimeona kabisa hapa kuna kitu kipya,”

Aliongeza, “Unajua ngoma nyingi za Chidi ambazo amekuwa akizitoa hivi karibuni sio level zake, lakini alivyonisikilizisha huu wimbo nimeona kuna kitu cha ziada kipo. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna jiwe linakuja,”

Meneja huyo amesema muda si mrefu wataanza kutangaza mfumo mzima wa uongozi wa rapa huyo.