Update:

Barrick kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjua dhahabu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold ya Canada, Profesa John Thornton amesema atashirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu hapa nchini (smelter). Profesa Thornton ameyasema hayo leo (Jumatano) Ikulu alipokutana na Rais John Magufuli kwa ajili ya kujadiliana kuhusu sakata la mchanga wa madini. Pia, Profesa Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania

No comments