Update:

Waziri nchini India ahimiza wanawake kupiga waume zao


Waziri nchini India ahimiza wanawake kupiga waume zao
Waziri mmoja wa India awatunuku ma biharusi magongo ya mbao katika hafla kubwa ya harusi ya halaiki na kuhimiza wanawake kuwapiga wanaume wao iwapo watawanyanyasa kwa kuwapiga au wakilewa .
Gongo hilo la mbao maarufu kama 'mogris' nchini humo lilikuwa na maandishi ya "zawadi kupiga wanaume wanaolewa".
Gopal Bhargava ni waziri katika jimbo la kati la Madhya Pradesh siku ya Jumamosi alitunuku mabibi harusi takriban marungu 700 katika hafla kubwa ya harusi ya halaiki iliyofanywa kwa ajili ya wanandoa walio maskini katika mkoa wa Grahakota.
Waziri huyo pia alibainisha kuwa endapo mwanamke atakuwa anampiga mumewe kwa rungu polisi hawataingilia kati.
Waziri huyo amefahamisha kuwa ni mbinu mojawapo zitakazotumika kupunguza unyanyasaji wa wanaume kwa wanawake wao hasa wakiwa wamelewa .

No comments