Update:

Vituo kumi vya polisi vyafekewa umeme na Tanesco

 Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limezidi kuviandama vitengo vya Wizara ya Mambo ya Ndani, baada ya kukatia umeme jumla ya vituo vya polisi 10 sambamba na ofisi ya usalama barabarani Mkoa wa Arusha. Juzi shirika hilo lilikata umeme kwenye ofisi na maduka ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), JKT Oljoro, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha pamoja na nyumbani wa Kamanda wa Polisi Mkoa sambamba na Magereza. Tanesco imeendeleza operesheni yake leo kwa kuwakatia umeme vituo vidogo vya polisi na Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWSA). Ofisa Uhusiano wa Tanesco, Saidy Mremi ametaja vituo vilivyokatiwa umeme kuwa ni pamoja na vituo vikuu vya kata ya Ngarenaro, Unga LTD, Sakina, Ngaramtoni, Sekei pamoja na Fire, Kijenge, Chekereni, Olorieni na Mbauda.

No comments