Update:

Tshabalala mchezaji bora ligi kuu Mei, awabwaga Niyonzima na Shaabani Idd


Bekia Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala' amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzaniua Bara wa mwezi Mei kwa msimu wa 2016/2017.
Hussein aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC.
Katika mwezi Mei kulikuwa na raundi 3 ambazo Hussein alicheza kwa dakika zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake kubaki katika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.
Pia alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopewa onyo la aina yoyote.

No comments