Update:

SIMULIZI: MWIBA WA PENZI SEHEMU YA KWANZA MTUNZI: GADIEL KITOMARY MWANDISHI: GADIEL KITOMARY MANDHARI: MOSHI-TANZANIA +255 673 530 592.

Image may contain: 1 person, closeup
Ndugu zangu jamaa na marafiki nawasalimu wote kwa pamoja,napenda kuja mbele yenu na hii simulizi ya MWIBA WA PENZI nikiwa na nia ya sisi kujifunza kuhusu mahusiano.Lakini awali ya yote napenda kumshukuru mwenyenzi Mungu kwa hali na nafasi aliyotupa mimi na wewe mpenzi msomaji pia nitambue uwepo wa CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA (AJTC) kwa mafunzo mazuri yenye kujenga fikra pana kwa kila muhitimu lakini pia sijawasahau wadau wangu wote wanaotoa maoni yao kwa kupitia ukurasa wangu huu,Mungu awabariki nyote kwapamoja.
#MWANZO
Halikuwa jambo lakuzoeleka machoni pangu kila nilipojaribu kulivumilia sikuweza… “Ni jambo la kawaida kwa wapendanao kuheshimiana na kuvumiliana hata visivyo vumilika ikiaminika ipo siku vitarekebishika vile vyote ambayo aviko sawa lakini kimtizamo inaonekana sisi wanawake tunaweza kuvumilia jambo baya ndani ya moyo wetu kuliko wanaume”…Nilikuwa nafikiria maneno hayo nikiwa sebuleni ghafla nilisikia oni ya gari nje ya geti nikaangalia saa ya ukutani ilikuwa saa nane za usiku kabla sijajisogeza niliwaza mume wangu ametoka wapi saa hizi na pia kwanini hata simu yake isipatikane mara nilisikia oni kwa mara ya pili nikachukua kanga nikajifunga nikafungua mlango nakuelekea getini kumfungulia mume wangu ninayempenda sana.
Nilipofika getini nilichungulia nikaona kuwa gari lililoko nje ni la mume wangu kipenzi basi nilifungua geti,Mume wangu akanisalimia akiwa yupo ndani ya gari akaelekea parking kupaki...baada ya mimi kufunga geti nilianza kupiga hatua kumfuata mme wangu ili tu akishuka ndani ya gari nimkumbatie kama ilivyo kawaida yangu japokuwa alichelewa kuja nyumbani lakini bado haikuwa sababu ya mimi kutokumuonyesha uwepo wangu… nilipomfikia mume wangu nilimpa pole kwa sauti chini huku nikiwa nimemkumbatia kiukweli sikuweza kujizuia machozi yalinitoka nikamwambia… mume wangu ulikuwa wapi hadi usiku wote huu jamani alafu pia hata simu yako haipatikani…akanijibu “samahani mke wangu nilikuwa kwenye kikao na wanasheria wenzangu si unajua ile kesi ya Abdalah inasomwa kesho” nikamuliza simu je vipi nayo kwanini haipatikani… akanijibu “simu niliacha kwenye gari alafu pia haikuwa na chaji kukakuwepo na baadhi ya watu walinipigia hadi simu ikazima,niliporudi ndani ya gari ndiyo nikaiweka chaji na muda huu ndiyo kama unavyoona imeingiza asilimia kumi” nilimtizama mume wangu usoni kwa umakini sikuwa na neno lakumuliza basi nilishusha mikono yangu katika mabega yake nikamshika mkono tukaelekea ndani….
Tulipofika ndani mume wangu aliingia bafuni kuoga na mara baada yakuoga nilimtengea chakula akala basi tukaelekea kulala na mume wangu kipenzi cha roho yangu hatimaye kulipambazuka,nikaamka nikapasha maji wakati maji yakiwa jikoni niliendelea kuandaa nguo zangu naza mume wangu…baada yakumaliza kuandaa nguo nilipeleka maji bafuni nikarudi kumuamsha mume wangu basi aliamka tukaenda kuoga wote tulipotoka bafuni mume wangu alikuta simu yake inaita kuangalia namba haikuwa na jina mume wangu akasema “huyu nani ananisumbua asubuhi hii”wakati huo ameshikilia simu kama anataka kupokea… nikamwambia pokea uwezi jua basi bila hiyana alipokea simu ghafla nilisikia sauti ya mwanamke ikisema hivi “baby hiyo ndiyo namba yangu ya tigo nimeshindwa kukupigia kwa voda yangu kwakua haina muda wa maongezi..umeamkaje baby wangu?” mume wangu akaguna akamuliza mpiga simu “unajua unaongea na nani?” jibu la mpiga simu “heee hata sauti unashindwa kuitambua wewe si Jastine?” ghafla mawasiliano yalikatika…..
Nikamuliza ni nani huyo uliyeongea naye mme wa wangu akanijibu huku akiendelea kujifuta maji kwa taulo “nafkiri huyu atakuwa amekosea namba tu mke wangu ondoa shaka juu yangu” nikamuliza kama amekosea namba hata na jina lako pia!!! Hapana mume wangu utakuwa umeanzisha mahusiano mengine nje kweli haiwezekani iwe hivyo kama ni kweli mpigie simu nimsikie akidhibitisha hilo mme wangu… hakuna kitu kibaya ambacho nakichukia kama kushea mume lakini kama umenichoka niambie tu mume wangu na siyo kunitesa sitaki kuumizwa na mapenzi mimi…nilimwambia mume wangu huku machozi yakinitoka pamoja na hivyo mume wangu hakuongea chochote.baada ya dakika chache mimi nikiwa sijaweza kufanya chochote mume wangu alimaliza kuvaa akaniaga nakuniambia kuna sehemu anapitia hivyo hatoweza kunisubiri nivae alafu anipitishe kazini kwangu basi sikumjibu chochote akafungua mlango akaondoka akaniacha ndani nikiwa na machungu mno.
Nilifungua kabati la nguo huku machozi yakishuka mashavuni mwangu nikachukua nguo nikavaa baada ya kuvaa niliondoka kuelekea kazini,nikiwa kwenye daladala niliwaza kuhusu mahusiano yangu na Jastine “ni muda mfupi tu umepita toka nimefunga harusi na Justine inakuwaje leo hii ameanza kunisaliti au nimfanyie nini huyu mwanaume” ghafla iliingia sms kwenye simu yangu kutoka kwa mume wangu ikisema “samahani mke wangu naomba kuhusu habari ya simu iliyopigwa asubuhi iishe tu tambua nakupenda sana baby wangu” baada yakusoma ujumbe huo niliguna nikachukua simu yangu nikairudisha kwenye pochi yangu kumbe wakati nairudisha simu yangu kwenye pochi ilikuwa haina mlio wala mtetemo.
Baada ya muda mfupi nilifika kazini nikasaini hatimaye nikaingia ofsini kwangu,nikafungua pochi yangu ili kuchukua laptop yangu ghafla niliona simu ikiwa inamwanga ikiashiria kuna sms imeingia au call bila mimi kusikia…nikaichukua simu mara nikaona kuna namba ngeni imenipigia mara nne… ghafla wakati huo huo ikapiga tena nikiwa nimeshika simu nikasikia sauti iliyosikika kama inatoka kwakulazimishwa “mke wangu Tina niii….” Mara simu ilikatika ghafla………
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA …………..CHAKUFANYA KAA KARIBU#NAKULIKE UKURASA  WA Fcebook  #DuniaLeo.