Update:

Simba yakanusha habari za kusuia tuzo

Siku moja baada ya tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kufanyika na kutoa zawadi kwa wahusika, timu ya Simba ambayo ni mshindi wa pili haikuwepo wala kutuma muhusika katika eneo la tukio ikihisiwa kuwa ni muendelezo wa kugomea zawadi ya mshindi wa pili.
Jana ziliripotiwa habari za uongo katika mitandao ya kijamii kuwa wekundu wa Msimbazi Simba kupitia kwa Rais wao Evans Aveva wamekubali nafasi ya mshindi wa pili na kufuta malalamiko yao FIFA kuhusiana na TFF kuituhumu kutotenda haki.
Akikanusha habari hizo Makamu wa Rais wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wao wapo nje ya mji wa Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya fainali yao dhidi ya Mbao FC na si kweli kwamba wamesusia tuzo.
Pamoja na hayo, Kaburu amesema timu yake imejiandaa vizuri katika fainali hiyo ili waweze kuchukua ubingwa na kuweza kuwakalisha nchi katika mashindano ya kimataifa.