Update:

Simba ya Tanzania kuwatema wachezaji saba wa kigeni


Wanamsimbazi na hata baadhi ya viongozi mpaka sasa hawaamini kama timu yao imeukosa ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara msimu huu, lakini mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo, Hamis Kilomoni amefichua siri nzito kuwa kuna wachezaji watano wa kigeni watatemwa na klabu hiyo ili kupisha wazawa kuipigania klabu hiyo kwani wanagharama ndogo na wanajitoa kuipigania timu kwa jasho na damu.Kilomoni aliyewahi kuwa mchezaji na kiongozi wa Simba kabla ya kuwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini, alisema Simba haikupata huduma sahihi kwa nyota wake saba wa kigeni iliowasajili msimu huu kwa uwezo mdogo walionao, hivyo anaona ni bora idadi yao ipunguzwe ibaki wawili tu.
Alisema mabosi wa Simba walifanya kosa kubwa kuwadharau wachezaji wazawa na kuwakimbilia wageni ambao wamekuwa hawana msaada wowote zaidi ya kuitia gharama kubwa ya kuwahudumia..
Hata hivyo Kilomoni hajawataja nyota wanaostahili kusalia, japo Simba kwa sasa ina wachezaji wa kigeni ambao ni Method Mwanjali, Juuko Murshid, Fredrick Blagnon, Janvier Bokungu, Laudit Mavugo, James Kotei na kipa Daniel Agyei.