Update:

SHAMBA LA MPUNGA LA WANANCHI LA MWASHKAMILE WALIPA FAINI NA KUFUNGULIWA MAJI.

Shamba la Wananchi lililoko katika wilaya ya Mbarali katika kata ya Kapunga ambalo limekuwa liktumia maji kwa muda wote bila ya kuyalipia chochote Serikalini lijulikanalo kama Mwashikamile lenye ukubwa wa ekari 800 limepewa ruhusa ya kufungua mfereji wa maji uliokuwa umefungwa baada ya Shamba hilo kulipa madeni yote ya maji na kulipa faini waliyopigwa na Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru Mto Ruaha.


Akiongea na Wananchi wa eneo hilo la mwashikamile Mwenyekiti wa Kikosi kazi hiko Bwana Richard Muyungi amewahimiza viongozi wa shamba hilo kuhakikisha hawaenedelei kuchepush mifereji ya maji bila kuyalipia na kutekeleza maagizo ya serikali ya kupata vibali vote halal vya matumizi ya maji na kilimo cha umwagilaji. Kikosi kazi kimewaruhusu Wananchi kuendelea na umwagiliaji wa maji katika mashamba yao ya Mpunga mpaka pale watakapovuna.


Bwana Muyungi alisisitiza kuwa hakuna wananchi wote wameruhusiwa kuendelea kutumia maji hadi kuhakikisha kuwa mazao yote mashambani yanavunwa la msingi ni kuea maji hayo wayalipie. Alsema wananchi katika mashamba memgi tayari wamekwishatoa michango ya kulipia maji lakini viongozi hawataki kulipia maji jambo ambalo haliwezi kuvumilika.


Aidha akiongea, Mwenyekiti wa eneo hilo la Mwashikamile Bwana Leonard Mwashikamile ameshukuru sana Kikosi kazi kwa kuwaruhusu tena kufungua mfereji wa maji na pia aliahidi kwa niaba ya Wananchi wa kijiji hicho kutunza maji yote yanayotumika kwa umwagiliaji na kuwa atahakikisha Wananchi hawachepushi maji ya wizi tena.


Shamba la Mwashikamile lilikuwa ni moja kati ya mashamba pamoja na skimu za umwagiliaji zilizopigwa faini na Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha katokana na kuchepusha maji bila kuyalipia na bila kibali chochote..

Pichani Wananchi wa Kijiji cha Mwasikamile ambao ni Wakulima wa mashamba ya mpunga ya Mwashikamile wakishirikiana kwa pamoja kufungua mfereji wa kupitishia maji ili kumwagilia mashamba yao baada ya kulipa faini waliyotozwa na Kikosi kazi cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha.
Mwenyekiti wa Kikosi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha Bwna Richard Muyungi akiongea na Wakulima wa mashammba ya Mpunga ya Mwashikamile mara baada ya kuzuru shambani hapo.

No comments