Update:

Polisi wanne wajeruhiwa kwenye maandamano ya siku ya wafanyakazi UfaransaWizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa imesema vuguru zilizotokea jana katika maandamano ya siku ya wafanyakazi mjini Paris, zimesababisha polisi wanne kujeruhiwa, wawili wao wamejeruhiwa vibaya.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bw Matthias Fekl amelaani vikali vurugu hizo dhidi ya polisi, na kuahidi kufanya juhudi zote kuwakamata wahusika waliowarushia mabomu ya petroli polisi.

Habari kutoka Paris pia zinasema kutokana na tishio la ugaidi, polisi na askari elfu tisa waliitwa jana, na elfu mbili kati yao kwa ajili ya kulinda usalama wakati wa maandamano mjini Paris.

No comments