Update:

Polisi nchini Kenya yawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mashambulizi

Vikosi vya usalama nchini Kenya vinawahoji watu wawili muhimu wanaotuhumiwa kuhusika na matukio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni katika kaunti za Garissa na Mandera, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wiki mbili zilizopita.
Ofisa wa serikali wa eneo hilo Mohamud Saleh amesema, watuhumiwa hao wanahojiwa na timu ya pamoja ya usalama kutoka polisi, jeshi, na upelelezi.
Askari polisi wanane waliuawa katika mashambulizi mawili tofauti ya kigaidi katika kaunti za Mandera na Garissa hapo jana wakati magari yao yalipolipuka baada ya kukanyaga mabomu yaliyotegwa ardhini.
Wakati huohuo, askari polisi wawili wa Kenya wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa mapema leo baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa ardhini katika kaunti ya Garissa iliyoko kwenye eneo la mpaka wa Kenya na Somalia.
Saleh amelituhumu kundi la Al Shabaab kwa kuongezeka kwa mashambulizi katika eneo hilo.

No comments