Update:

Papa aingia kwenye boti na kumjeruhi mvuvi AUSTRALIA


mvuvi


Mvuvi mmoja nchini Australia ameelezea jinsi papa mwenye uzito kilo 200 alivyoruka ndani ya boti lake na kumjeruhi mkono.

Terry Selwood mwenye umri wa miaka 73 aliacha maelezo kwenye ofisi zao zilizopo New South Wales, kama ilivyo kawaida pindi mnyama anapotoka mwenyewe kwenye maji.

Selwood anasema papa huyo alikuwa na urefu wa mita 2.7 na aliingia kwenye boti lake lenye urefu wa mita tano na kumjeruhi kwa kutumia sehemu yake ya upanga.

Selwood aliokolewa mara baada ya kupiga kelele za kuomba msaada.

''Nilipoteza damu nyingi, nilipata mshtuko na kupoteza fahamu na kumfikiria Mungu. Siamini kama nimetoka nikiwa hai,'' alieleza Selwwod kwenye chombo cha habari cha Australia, Australian Broadcasting Corp (ABC).