Update:

MWIBA WA PENZI SEHEMU YA PILI (2)

SIMULIZI: MWIBA WA PENZI
SEHEMU YA PILI (2)
MTUNZI: GADIEL KITOMARY
MWANDISHI: GADIEL KITOMARY
MANDHARI: MOSHI-TANZANIA
+255 673 530 592.
Nina furaha kubwa sana kutokana ushirikiano wako wewe mpenzi msomaji wa simulizi zangu hivyo basi endelea kutoa maoni yako na kulike kadri utakavyo weza, kwani ni sehemu ya kuleta faraja kwangu na kunitia moyo juu ya kile ninahokileta kwako, lakini awali ya yote tumshukuru Mungu kwa siku ya leo tena kwa kutupa nguvu na uheledi wakufanya kazi zetu kiusahihi pia nitambue uwepo wa #CHUO_CHA_UANDISHI_WA_HABARI_NA_UTANGAZAJI_ARUSHA_(AJTC) kwakutoa taaluma bora hapa Tanzania.
Related image
#MWENDELEZO (2).
Baada ya simu kukatika nilishikwa na butwaa “kulikoni mme wangu amenipigia simu na namba nyingine mpya au simu yake imefanyaje?” nilikuwa najiuliza huku nikiendelea kumpigia mme wangu kupitia simu yake yamkononi,ghafla baada ya sekunde kadhaa niliambiwa namba haipatikani...nikapiga kupitia namba mpya nikambiwa namba inatumika,duh!! Niliumia sana nikaamua kukaa huku hisia za mwili wangu zikishindwa kutafasiri nini kinachoendelea,nikarudia tena kupiga namba mpya hakika sikuamini niliambiwa namba haipatikani,nilinyanyuka kwenye kiti nikaanza kuelekea ofisini kwa meneja ili niweze kuomba ruhusa niondoke niende nyumbani huku nikiwa na imani mpaka nikifike nyumbani nitakuwa nimejua nini kinacho endelea,nilipofika mlangoni mwa ofisi ya Meneja niligonga hatimaye ilionekana ndani hapakuwepo na mtu hapo hapo nikawaza kumpigia Meneja simu kuangalia mikono yangu sikuwa na simu kumbe nimeiacha mezani ofisini kwangu,nikaanza kuelekea ofisini kwangu upesi ili nikampigie Meneja…zikiwa zimebaki kama hatua tatu kuufikia mlango wa ofisi yangu alikuja mhazili (secretary) akiwa na na hali ya haraka kupita kiasi akapaza sauti akaniambia “Dada Tina kuna mtu anauhitaji wa kukuona kwa uharaka yuko mapokezi” nikamjibu mwambie aje,basi mimi nikaingia ofisini kwangu.
Baada ya mimi kuingia ofisi nilichukua simu nikampigia Meneja kwa bahati nzuri akapatikana hewani na hatimye alipokea simu yangu “Habari za asubuhi meneja” akanijibu salamu yangu “Salama namshukuru Mungu ni mwema” nikadakia juu juu kwa haraka haraka nikamwambia…Meneja kuna tatizo la kifamilia limejitokeza naomba nirudi nyumbani kwa siku ya leo,Meneja aliniruhusu huku akitaka kujua tatizo langu kulingana na hali ya mawasiliano yangu mimi na yeye yalivyokuwa kwa wakati huo lakini nilimuahidi nitamwambia baadae,wakati nikizungumza na simu mlango ulikuwa unagongwa ishara ya kubishwa hodi nikaruhusu aliyekuwa anagonga aingie hatimaye mlango ulisukumwa macho yangu yakawa yanatizama mlangoni nikisubiri anayeingia ni nani…sikuamini macho yangu aliyeingia ofisini kwangu ni Shemeji yangu,hapo hapo nilihisi kuna jambo siyo kawaida shemeji yangu kuja ofisini bila kunipigia simu,tulisalimiana na shemeji yangu huku nikimuona akipepesa macho kwa woga wakutaka kuzungumza jambo lakini inaonekana nafsi yake ikisita,mara shemeji yangu alianza kuzungumza “Shemeji nimekuja hapa kukutaka uombe ruhusa kuna jambo limejitokeza ghafla” nilishtuka sana huku mkono wangu ukichukua simu nakumpigia mume wangu hakika bado simu haikupatikana, nikamuliza shemeji yangu huku nikiwa na hofu kubwa kuhusu mume wangu… shemejiii nambie ni nini hicho kilichotokea akanijibu “Kaka yangu ambaye ndiye mume wako amepata ajali na kwasasa yuko KCMC Hospital” sikuamini masikioni kwangu nilichoambiwa kuhusu mume wangu kipenzi,nikasimama kwenye kiti huku nikihisi kuishiwa nguvu za mwili nikamkaribia shemeji yangu nakumuliza tena kweli Mume wangu amepata ajali akanijibu “ndiyo” sikuweza kuongeza neno,tulitoka na shemeji yangu kuelekea KCMC Hospital…wakati tukiwa njiani nilikumbuka sauti yake iliyotoka kwakulazimishwa pale alivyonipigia simu kwa namba mpya ikisema hivi “Mke wangu Tina nii” ghafla simu ile ilikatika,baada ya kukumbuka tukio lile nililia sana ndani ya gari nilitamani mawasiliano yasingekatika nijue ni nini ambacho Mume wangu alitaka kuniambia kwa wakati ule ingawaje kwasasa nimepata taarifa kuwa amepata ajali.
Baada ya muda mfupi tulifika KCMC Hosipital nikiwa na shemeji yangu..tukashuka kwenye gari tukaanza kuelekea wodini alipokuwa mume wangu… tulipofika kwenye mlango wa chumba alichokuwa mume wangu ghafla tu ile hali ya shemeji yangu anaelekeza mkono mlangoni teyari kufungua mlango mara ukafunguliwa na binti mmoja aliyekuwa ndani mwa chumba hicho huku akiwa ameshikilia leso machoni kwakufuta machozi akilia mno…ghafla aliondoa leso usoni hakika sikuamini nilichokiona mbele yangu na sijuhi ndani kukoje…..
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA………..CHAKUFANYA KAA KARIBU KWA #KULIKE UKURASA HUU WA #DuniaLeo ILI CHAPISHO JIPYA LIKITOKA TU HAPO KESHO KUTWA ALHAMISI TAR 4/05 UWE WAKWANZA KULIPATA.
******************************
#MAONI YAKO NI MUHIMU KWANGU.

No comments