Update:

Muendesha Pikipiki Nicky Hayden apata ajali mbaya mazoezini

Image result for Nicky Hayden


Muendesha Pikipiki mashuhuri nchini Marekani, Nicky Hayden, amepata ajali, baada ya kugongwa na Gari alipokuwa akifanya mazoezi ya kuendesha pikipiki yake. Bingwa wa dunia wa mchezo huo amesema kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya magharibi mwa Rimini. Hayden, alikuwa nchini Italia na kwa sasa amefikishwa hospitali ya jamii iliyopo karibu na maeneo hayo kwa matibabu zaidi. Habari zinaeleza kuwa Mchezaji huyo wa Pikipiki ameumia zaidi maeneo ya kichwani pamoja na kifuani na hivyo yupo katika hali mbaya. Hayden, mwenye umri wa miaka 35 amewahi kushinda ubingwa wa Mchezo wa kukimbiza Pikipiki 'MotoGP ' mwaka 2006.