Update:

Mtoto aliyezaliwa na miguu mitatu Bangladesh afanyiwa upasuaji Australia

Mtoto mmoja aliyetajwa kwa jina la Choity Khatun (3) Nchini Bangladesh aliyezaliwa akiwa na miguu mitatu amefanyiwa upasuaji nchini Australia na sasa anarudishwa nyumbani
mtoto huyo alizaliwa na ulemavu huo ambapo mguu huo ulikuwa umemea katika mfupa wake wa kiuno.
Wapasuaji wa Australia walitumia mwezi mmoja wakifanya kazi ya kuuondoa mguu huo na kurekebisha eneo lake la mfupa wa kiunoni.
Daktari Chris Kimber ,kiongozi wa upasuaji katika hospitali ya Monash huko Victoria alisema kuwa kesi ya Choite ilikuwa isio ya kawaida na kwamba upasuaji huo ulikuwa mgumu.
”Upasuaji hutegemea mtu anayefanyiwa na lazima utumie muda mwingi kuchanganua ni nini kilichopo na baadaye upange mpango unaoshirikisha hayo yote”, aliambia kituo cha habari cha Australia Broadcasting Cooperation.

No comments