Update:

MBAO FC TAYARI IPO JIJINI DAR ES SALAM KUIKABILI SIMBA KOMBE LA TFF

Na Clement shari
Timu ya soka ya Mbao Fc ya jijini Mwanza tayari kabisa imeshatua huko Jijini Dar Es salaam kuelekea pambano lao la Jumamosi hii la ligi kuu ya kandanda Tanzania bara VPL litakalopigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi kuanzia mishale ya saa moja kamili usiku.
Msemaji wa Mbao Fc Cristant Malinzi ameiambia Masacky Media kwa njia ya simu kuwa timu imetua jijini Dar Es Salaam ikiwa tayari tayari kwa ajili ya pambano hilo ambapo amesema vijana wake wamejiandaa vya kutosha kuelekea pambano hilo na wameahidi kufanya vizuri.
Malinzi amesema katika kikosi cha Mbao hakuna majeruhi yeyote na wanachosubiria ni muda tu ufike waingie uwanjani kuchukua pointi 3 muhimu.
Kwa ujumla ligi kuu inataraji kuendelea weekend hii kwa baadhi ya viwanja kuwa katika wakati mgumu ambapo Jumamosi Mei 6 kunataraji kuwa na mechi tano.
Kwa mujjibu wa ratiba, Michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza  wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.