Update:

Majeruhi wa Lucky Vincent wazungumza kwa mara ya kwanza wakiwa wodini Marekani

Madaktari wa Hospitali ya Mercy, ya Marekani wamesema watoto  watatu majeruhi wa ajali ya Lucky Vincent, wanaendelea vyema.
Kwa mujibu wa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa hali zao kwa sasa zinatia tumaini.
Katika ukurasa wake wa faceboook , Nyalandu ameandika kuwa watoto Saidia Ismael, Doreen Mshana na Wilson Tarimo  watapelekwa katika makazi maalum ya kuangalia afya zao ikiwa ni pamoja na kupewa mazoezi ya viungo.
Hata hivyo, Nyalandu ameandika kuwa watoto hao  wataendelea kuwa katika wodi ya watoto huko  Mercy  Hospital  hadi madaktari bingwa watakapojiridhisha  na hali yao.