Update:

MAANDAMANO YA MAGARI YAFUTWA GHAFLA!Maandamano ya magari yamefutwa katika maadhimisho ya siku ya Mei Mosi kutokana na umati mkubwa wa wafanyakazi na wananchi waliojitokeza Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kwenye sherehe hizo.

Magari hayo yalikuwa yaanze kuingia uwanjani hapo saa 5:00 asubuhi leo baada ya maandamano ya wafanyakazi na mabango kupita mbele ya Rais John Magufuli kumalizika lakini umati wa watu umefanya waandaji kuyafuta.

Mshereheshaji katika sherehe hizo pamoja na polisi na vijana wa skauti kujitahidi kurejesha watu nyuma ili maandamano ya magari yapite, zilishindikana. Badala yake, yalipita maandamano ya walimu ambayo yaliwekewa utaratibu maalum wa kuingia tofauti na makundi ya wafanyakazi wengine.