Update:

Maamuzi ya JPM kwa viongozi walioomba kuacha kazi, yupo RC Meck SadickKurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Dar es salaam imeeleza kuwa Rais Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa Said Meck Sadick aliyekuwa RC Kilimanjaro, Aloysius Kabulizi na Upendo Hillary Msuya waliokuwa Majaji wa Mahakama Kuu.

Taarifa iliyotumwa na Kitengo cha mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema mwingine aliyeomba kuacha kazi ni Upendo Msuya aliyekuwa Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo May 16, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imesema Rais Magufuli ameridhia maombi hayo kuanzia May 15, 2017.

No comments