Update:

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya: Juventus yatinga fainali

Juventus imefanikiwa kutinga fainali ya ligi ya mabingwa ulaya ikiwa ni timu ya kwanza kufanya hivyo mzimu huu. Juventus ilikutana jana na AS Monaco na kuwachabanga magoli 2-1 hivyo kuvuka kwa jumla ya magoli 4-1 baada ya ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali.
Magoli ya Juve yaliwekwa kimiani na Mandzukic na Dani Alves, na Monoca kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na kinda Kylian Mbappe.
Leo kunachezwa mechi nyingine ya nusu fainali ya pili kati ya Real Madrid na Atletico Madrid ambao watakuwa nyumbani Vicente Calderon. Atletico leo itawapasa kufunga jumla ya magoli 4 -0 ili kufuzu kuingia fainali.
Kocha Dieogo Simeone amesema anawaamini wachezaji wake kwani wanajua nini wanaweza kufanya.

No comments