Update:

WAANDISHI WA HABARI ZAIDI YA NANEMKOANI ARUSHA AKIWEMO MEYA WA JIJI HILO WAACHIWA HURU
Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wameachiwa huru mara baada ya kuwekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Tukio hilo ambalo liliamsha hisia za waandishi mkoani hapa limetokea katika mazingira ambayo bado hayajatolewa ufafanuzi. Kwa mujibu wa maelezo ya awali ya ki Upelelezi yalisema kuwa watuhumiwa hao waliwekwa chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.Miongoni mwa waliokamatwa ni Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10. Viongozi wa dini bado wanaendelea kuhojiwa.Jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kupitia kaimu Kamanda Yusuph Ilembo amesema hakukamata mwandishi yoyoyte bali walipewa lifti