Update:

Kuelekea CAN 2019, timu ya Taifa ya DRC kuanza mazoezi ikijiandaa kwa mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Jamhuri ya Congo

wachezaji 28 wa timu ya taifa ya DRC wameitwa kwa ajili ya kuanza mazoezi Mei 25 kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Red Devils ya Jamhuri ya Congo.
Mchezo huo umepangwa kufanyika Juni 10 mjini Kinshasa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufuzu michuano ya CAN 2019 Uliopangwa kufanyika ya June 10 jijini Kinshasa.
Mratibu wa timu ya taifa ya DRC Theobald Binamungu, amesema DRC Kocha wa timu hiyo Florent Ibenge Ikwange, ameita wachezaji hao ili kuanza mazoezi mara moja kujiandaa na mchezo huo.
DRC imepangwa kundi G la kufuzu katika michuano ya CAN yatakayofanyika nchini Cameroon mwaka 2019, timu zingine katika kundi hilo ni Congo, Zimbabwe na Liberia.