Update:

KLM kugharamia safari ya kurudi ya wanafunzi wa Lucky Vincent

Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ya jijini hapa waliosafirishwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu, watarejea nchini pamoja na waliowasindikiza kwa usafiri wa bure uliotolewa na Shirika la Ndege la Uholanzi(KLM) Wanafunzi waliosafirishwa ni Sadia Awadh,Wilson Tarimo na Doreen Elibarick kila mmoja akiwa na mama yake, muuguzi na daktari bingwa wa mifupa ambao waliondoka nchini tangu Mei 14, mwaka huu Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyewezesha safari ya kwenda Marekani kupitia taasisi Stemm ambayo ni mwenyekiti mwenza, amesema kuwa usafiri huo uko tayari muda wowote matibabu ya wanafunzi hao yatakapokuwa yamekamilika. "Napenda kuthibitishia kuwa usafiri wa kurudi upo jambo la muhimu Watanzania wote tumwombe Mungu wapate nafuu kwa haraka baada ya upasuaji waliofanyiwa ili waweze kuendelea na masomo yao,"amesema Nyalandu.

No comments