Update:

Kisa soka mashabiki wapigana risasi na mmoja kufariki.Hakika soka ni mchezo wa kuvutia na uliojaa msisimko wa kila aina haswa linapokuja suala la upinzani, kila shabiki wa timu hapendi kuzidiwa na shabiki wa timu nyingine.

Huko nchini Argentina mshabiki mmoja wa klabu ya Newell’s Old Boys amejikuta matatizoni baada ya kuwapiga risasi watu wawili wakiwa katika ubishani wa masuala ya mpira.

Kijana anayekadiriwa kuwa na miaka 17 amekamatwa na polisi baada ya kumfyatulia risasi mzee mmoja na mwanamke mwingine baada ya kushindwa katika mabishano.

Inasemeka kijana huyo alimpiga risasi ya kifua mzee huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 44 na alifariki wakati akiwa njiani kupelekwa hospitali huku mwanamke aliyepigwa risasi hali yake ikiwa sio nzuri kiafya.

Newell’s Old Boys na Rosario Central ni wapinzani wakubwa nchini Argentina na walikutana mwishoni mwa wiki wakati Rosario Central wakiibuka kidedea ugenini kwa mabao 3 kwa sifuri.Matukio ya mashabiki kuuana nchini Argentina kutokana na soka yameanza kuonekana kama jambo la kawaida kwani katika msimu huu wakati wa mechi ya Belgarano na Tallers kuliibuka vurugu kubwa na shabiki akauwawa uwanjani.