Update:

Kenya yaongeza mshahara wa kima cha chini kwa asilimia 18


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 18, ili kuwapunguzia watu wenye mapato ya chini athari zinazotokana na mfumuko wa bei uliofikia asilimia 11.5 katika miezi 57 iliyopita.
Kwenye sherehe ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika Nairobi, rais Kenyatta amesema ongezeko hilo linalenga kupunguza matatizo yanayowakabili watu wa tabaka la chini nchini humo.
Rais Kenyatta pia ametoa amri ya kuongeza bonasi isiyotozwa kodi na malipo ya muda wa ziada hadi kufikia dola elfu 1 za kimarekani, ili kuwasaidia watu wenye mapato ya chini.

No comments