Update:

Kenya kuagiza mahindi kutoka nje ili kupunguza uhaba wa chukula


Kenya imepanga kuagiza tani laki 5 za mahindi kutoka Ethiopia, ili kupunguza uhaba wa chakula unaoendelea nchini humo.
Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Kenya Dkt Richard Lesiyampe amesema, jumamosi wiki hii mahindi hayo yatafikishwa kwenye wilaya ya Moyale kwenye mpaka kati ya Kenya na Ethiopia.
Uagizaji wa mahindi hayo ni sehemu ya mpango wa ruzuku wa serikali unaolenga kutoa mahindi ya bei nafuu kwa wateja, huku akiongeza kuwa katika wiki kadhaa zijazo, serikali itaagiza mahindi kutoka Zambia.
Habari nyingine zinasema, Shirika la Chakula na Kilimo cha Umoja wa Mataifa FAO na Shirika la Chakula cha Dunia WFP yametoa taarifa kuwa watu milioni 20 katika nchi nne za Afrika wanakabiliwa na njaa.
Taarifa imesema, watu walioko kaskazini mashariki mwa Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen wanakabiliwa na msukosuko mkubwa wa kibinadamu kutokana na ukame,na vita dhidi ya makundi ya kigaidi likiwemo kundi la Boko Haram na Al-Shabaab.

No comments