Update:

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeingia matatani baada ya kushindwa kulipa deni sugu

Related image
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeingia matatani baada ya kushindwa kulipa deni sugu la shilingi bilioni 1.2, inazodaiwa na mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira (AUWSA) ,kutokana na malimbikizo ya zaidi ya miaka 30  ya malipo  ya maji.

Mbali na jeshi hilo pia taasisi zingine za serikali mkoani hapa ni Hospitali  ya mkoa,  Mount Meru inayodaiwa zaidi ya sh, milioni 700.1, shule ya sekondari ya Arusha sh milioni 67,Magereza ,Uhamiaji na usalama wa Taifa.

Wadaiwa wengine ni Ikulu ndogo,ofisi ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ,Jiji la Arusha, mashirika ya Umma na binafsi , Wateja wa majumbani na viwandani ambapo kwa ujumla Auwsa inadai  kiasi cha shilingi billion 1.3.

Akizungumza jana na vyombo vya habari jijini Arusha,mwenyekiti wa bodi wa Auwsa,Job Laizer aliwataka wadaiwa sugu kujitokeza na kuanza  kulipa madeni yao mara moja kabla ya kuanza zoezi la kusitisha huduma ya maji mapema iwezekanavyo.