Update:

FEMATA”kugundulika kwa upotevu wa raslimali na mapato ya nchi,kutapelekea mabadiliko makubwa sana nchini”


SHIRIKISHO la Vyama vya wachimbaji madini Tanzania (FEMATA) limesema kwamba kugundulika kwa upotevu wa raslimali na mapato ya nchi,kutapelekea mabadiliko makubwa sana nchini.
RAISI wa Shirikisho hilo,BWANA JOHN BINA amesema hayo mjini Singida alipokuwa akimpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa hatua yake aliyoichukua kwa kuthubutu kuwaambia watanzania ukweli kwa sababu kitendo cha aina hiyo ni cha kizalendo na kishujaa.
AMESEMA BINA kuwa kitendo alichochukua Rais ni kitendo chenye manufaa kwa watanzania hususani wachimbaji wadogo wanaofanya biashara ya kusafirisha michanga kwenda nje,ambayo husafirisha michanga hiyo kama kopa lakini kumbe ndani yake kuna dhahabu.
NAYE Mtendaji Mkuu wa Wachimbaji wadogo Tanzania, BW.HARUNA KINEGA pamoja na kumpongeza Rais lakini akatumia fursa hiyo kuwaomba watendaji wote waliopo katika sekta ya Madini kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa moyo aliouonyesha.