Update:

Dkt. Joel Bendera: ''Wafanyabiashara zingatieni misingi ya sheria ,kanuni,na taratibu bila kuathiri upande wowote”


Wafanyabiashara Mkoani Manyara wametakiwa kufanya shughuli zao kwa kufuata misingi ya sheria, kanuni na taratibu bila kuathiri upande wowote.
Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Manyara Dkt. Joel Bendera kwenye mkutano wa wafanyabiashara ulioandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara (TCCIA) mkoa wa Manyara na kuwashirikisha Wadau mbalimbali wa mkoa.
Bendera alisema kuwa kwakuwa mkutano huo umelenga kuelimishana kuhusu sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji biashara, wafanyabiashara hao hawana budi kutimiza wajibu wao kwa Serikali kuu, Halmashauri za wilaya na Serikali za vijiji na mitaa.
Kwa upande wake Mshauri biashara TCCIA Ramadhani Msangi alisema kuwa uhusiano uliopo kati yao na taasisi  za serikali hauridhishi kutokana na taasisi hizo hasa TRA kutekeleza majukumu yao kwa njia ambayo imekuwa ikiwanyima uhuru wafanyabiashara.