Update:

Bw Emmanuel Macron aapishwa kuwa rais wa Ufaransa

Bw Emmanuel Macron ameapishwa rasmi kuwa rais wa Ufaransa na kuchukua nafasi kutoka kwa rais François Hollande anayemaliza muda wake.
Kabla ya kuapishwa kwake, mwenyekiti wa Kamati ya katiba ya Ufaransa Bw Laurent Fabius alitangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu na kumtangaza Bw. Macron kuwa rais mpya wa Ufaransa.
Akihutubia sherehe ya kuapishwa kwake, Bw Macron amesema atachukua hatua zote kuhimiza Ufaransa iwe na uhai na ustawi tena, na kuwafanya wananchi wake wawe na moyo wa kujiamini, pia kuendelea kuhimiza ujenzi wa Umoja wa Ulaya.
Ameongeza kwamba mgawanyiko wa aina yoyote wa kiuchumi, kijamii, kisiasa na kimaadili nchini Ufaransa utapunguzwa na kutatuliwa.