Update:

Balozi wa Tanzania Marekani kuwatembelea manusura wa Lucky Vicent leoBalozi wa Tanzania Marekani, Wilson Masilingi anatarajia kuwatembelea watoto watatu manusura wa ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya msingi ya Lucky Vicent walio nchini Marekani kwa matibabu.

Wanafunzi 32 walifariki katika ajali hiyo iliyotokea Karatu, Arusha. Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM) Lazaro Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa Balozi Masilingi atawatembelea watoto hao ili kuwajulia hali leo baadaye.

Nyalandu amesema watoto hao, Saidia Doreen na Wilson wapo Marekani kwa ajili ya matibabu na tayari wameshafanyiwa upasuaji na sasa wapo wodini.

No comments