Update:

23 wagundulika kuwa na kipindupindu Unguja

Wakati mvua za masika zikishika kasi na kuziathiri nyumba kadhaa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema watu 23 wamegundulika kwa na ugonjwa wa   kipindupindu.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Waziri wa Elimu, Riziki Pembe Juma amesema miongoni mwa watu hao yumo mtoto wa miezi mitatu na mzee mwenye miaka 75.
Riziki amesema waliobainika kuathirika na maradhi hayo ni wananchi kutoka wilaya za Mjini, Magharibi A, Magharibi B na Kaskazini A kwa upande wa Unguja na wilaya za Micheweni na Wete kisiwani Pemba.
Amesema kambi imefunguliwa Chumbuni na tathmini ya madaktari inaonyesha wagonjwa hao wameathiriwa kutokana na mazingira kuwa machafu kutokana na mvua iliyosababisha baadhi ya nyumba kuzungukwa na maji.

No comments