Update:

Zidane ataka La Pen kutopewa kura katika uchaguzi Ufaransa


Kiungo wa zamani wa ligi ya ulaya na kocha wa timu ya Real Madrid Zinedine Zidane amewataka wananchi wa Ufaransa kutompa kura mgombea urais kupitia chama cha mrengo wa kulia Marine Le PenKiungo wa zamani wa ligi ya ulaya na kocha wa timu ya Real Madrid Zinedine Zidane amewataka wananchi wa Ufaransa kutompa kura mgombea urais kupitia chama cha mrengo wa kulia Marine Le Pen.

Zinedine Zidane ambae aliwahi kuwa bingwa katika kombe la dunia na kombe la Ulaya amewahimiza raia wa Ufaransa kutoruhusu mtu kama Le Pen kuwa kiongozi wao.

Kwa mujibu wa habari,Zidane aliwahi kumpinga baba wa Marine Le Pen wakati alipofuzu kuingia katika raundi ya pili ya uchaguzi mwaka 2002.

Zidane ambae mpaka sasa ni maarufu sana Ufaransa amesema ya kuwa ujumbe aliotoa kuhusu Jean Marie Le Pen mwaka 2002 hauna utofauti na ujumbe wa sasa.

Le Pen anatarajia kuchuana vikali na Emmanuel Macron katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Mei 7.

No comments