Update:

Yanga yapeleka taarifa Takukuru na Polisi ili kufuatilia mwenendo wa utendaji kazi wa kamati ya saa 72 ya TFF

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema umepeleka taarifa kwenye taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru na Jeshi la Polisi ili kufuatilia mwenendo wa utendaji kazi wa kamati ya saa 72 ya TFF.
Mjumbe wa kamati tendaji ya Yanga, Salum Mkemi alisema wana wasiwasi na kamati hiyo inaweza kuipa Simba pointi tatu kutokana wajumbe wake wengi kuwa wanachama wa Simba.
Mkemi aliwataja wajumbe wa kamati hiyo Msafiri Mgoyi, Baruani Muhuza na Boniface Wambura aliodai ni wanachama wa kugalagala wa Simba hivyo uwepo wao katika kamati hiyo utaathiri maamuzi yatakayotolewa.
Hata hivyo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alisema viongozi wa Yanga wanataka kuharibu mpira kwa kuingilia utendaji wa kamati na Bodi ya Ligi.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa (TFF) Alfred Lucas alizitaka pande mbili kusubiri uamuzi utakaotolewa na kikao cha kamati kitakachoketi leo.

No comments