Update:

Watu 26 wafariki Dunia kwa ajali ya basi Nairobi

Takribani watu 26 wafariki katika ajali mbaya iliyohusisha basi la abiria na lori eneo la Kambuu katika makutano ya barabara ya Nairobi – Mombasa.
Kulingana na ripoti ya Polisi abiria wengine wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo la abiria liliokuwa likielekea Mombasa kujaribu kuyapita magari kadhaa na kugongana uso kwa uso na lori.

No comments