Update:

Watu 20 wafariki katika ghasia zilizozuka baina ya makabila mawili Kasai DR Congo


Watu 20 waauawa katika ghasia zilizozuka Kasai DR Congo

Watu 20 wafariki katka ghasia zilizozuka baina  ya makabila mawili Kasai DR Congo
Watu 20 wameripotiwa kufariki kufuatia ghasia zilizozuka bain aya  makabila mawili katika mkoa wa Kasia Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Taarifa hiyo imetolewa  Jumatano na  ujumbe wa Umoja wa Mataifa MONUSCO.
Msemaji wa MONUSCO mjini Kinshasa Hag Serge  katika mkutano na waandishi wa habari alifahamisha kuwa  watu 20 wa jamii ya Tshokwe-Pende  waliuawa Aprili 19  katika ghasia na jamii ya Lulua-Luba katika eneo la Mungamba kwenye umbali wa kilomita 30 mashariki mwa Tshipaka.
Naibu gavana wa  Kasai  Jean-Hubert Mbingho hajathibitisha ghasia hizo huku akikemea Umoja wa Mataifa kuonesha upendelevu katika taarifa yake.

No comments