Update:

Watano mikononi mwa polisi kwa uvuvi haramu

. Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watano wakazi wa Wilaya ya Sengerema kwa tuhuma za kukutwa na zana haramu za uvuvi kinyume cha sheria.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Watano-mikononi-mwa-polisi-kwa-u...
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amewataja watuhumiwa hao waliokamtwa saa 10:00 alfajiri ya Aprili 21 mwaka huu, kuwa ni Poneja Mkashi (51), mkazi wa kijiji cha Ngoma wilayani Sengerema na Simeo John (23) na Mashaka Hitila (17).
Wengine wanaoshikiliwa kwa mahojiano kabla ya kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa Kamanda Msangi ni Daniel Lucas (25) na Turuzila Hitila (35), wote wakiwa wakazi wa Kijiji cha Rubanda wilayani humo.
SOURCE:MWANANCHI

No comments