Update:

Wapinzani Nchini Venezuela wapanga kuendelea na maandamano

Wafuasi wa vyama vya upinzani Nchini VENEZUELA wapanga kuendelea leo na maandamano yalioanza jana ya kumshinikiza Rais Maduro kung’oka madarakani.
Polisi wa kuzuia ghasia walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wapinzani Jijini Caracas, ambapo kijana mmoja alipigwa risasi na kupoteza maisha.
Katika Mji wa magharibi mwa nchi hyo San Cristobal, mwanamke mmoja aliuawa mara baada ya maandamano kugeuka kuwa ghasia kubwa.
Upinzani unataka uchaguzi mpya wa urais kutokana na kudorora kwa hali ya chumi nchini humo.
Rais Maduro ameulaumu upande wa upinzani kwa kusababisha ghasia hizo.

No comments